JUHUDI ZAKE NDIO MAFANIKIO YA WANAWAKE WENGI KUINGIA KWENYE SIASA
TABORA
By Kisali Simba
https://youtu.be/r3YRUe3k48s?
Kutana na Bi Ashura Mwazembe, mwanamke jasiri anayesimama kama kiongozi wa wajasiriamali mkoani Tabora. Mbali na kuwa mjasiriamali hodari, pia ni mwanasiasa mwenye maono makubwa katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii. Kupitia juhudi zake, amewahamasisha wanawake kujikwamua kiuchumi na kushiriki kikamilifu katika demokrasia.