By Naomi Achieng
Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Mkoani Dodoma kupitia Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Bi. Maryrhobi Mabhaya wakati wa Kongamano la wakina mama lililofanyika mwishoni mwa wiki mkoani Dodoma kwa kauli moja limeipongeza Serikali kwa kuwezasha mazingira mazuri ya ukuaji wa kiuchumi wa wanawake pamoja na kuongeza fursa za kiuchumi.
Hivi sasa kuna fursa lukuki za kiuchumi ambazo wakinamama tukizitumia vizuri zitasaidia kubadilisha uchumi wa wakina mama wa Dodoma.Sisi kama Jukwaa malengo yetu ni kujenga eneo la maduka makubwa“Shopping Mall“ pamoja na kuwa na eneo maalum la biashara ta wakina mama“Alisema Maryrhobi
Mlezi wa Jukwaa *Mama Tunu Pinda* amesema ni wakati sasa wanawake wa Dodoma kutumia fursa hizi kubwa kiuchumi ambazo Mh. Rais Samia amekuwa kinara wake kuzitengeneza hapa Dodoma ili kujiimarisha na kukua zaidi kiuchumi.
kwa upande wake Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde amesema tangu maamuzi ya kuhamishia shughuli za serikali Dodoma,fursa nyingi za kiuchumi zimeongezeka na hivyo serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ili kuliona kundi kubwa la wanawake likinufaika kupitia sheria na sera wezeshi.
Aidha Mavunde ameongeza kuwa Mh. Rais Samia amerudisha mikopo ya wakina mama ya 10% na pia Sheria ya Manunuzi ya Umma imefanyiwa marekebisho ili Taasisi nunuzi zitenge 30% ya manunuzi yake kwa ajili ya makundi maalum likiwemo kundi la wakina mama.
“Nitaendelea kuunga mkono jitihada za kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa vitendo,na mwaka huu nitakabidhi kwa kikundi cha wakina Mama Ipagala mitambo ya kusafisha mafuta ya Alizeti ambapo ni sehemu ya ahadi yangu ya uanzishwaji wa kiwanda cha kuongeza thamani mazao kila mwaka“Alisema Mavunde
Wanawake hao pia wametumia jukwaa hilo kumpatia tuzo ya heshima Mhe. Mavunde kwa kutambua mchango wake mkubwa kuwaendeleza wakina mama mkoani Dodoma.