Baadhi ya wanawake wa eneo la Magogoni wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam Tanzania wakiwa pembezoni mwa bahari ya Hindi wakichambua zao la Mwani na kufunga katika Kamba tayari kwa ajili ya kupanda katika vitalu ambavyo wameviandaa ndani ya bahari hiyo.
Wanawake hawa wanasema zao hili la Mwani lina faida nyingi na ni chakula kizuri katika mwili wa binadamu kwani hutumika kutengeneza vitu mbalimbali ikiwemo Mafuta, sabuni, lishe ya uji wa mtoto, kachumbari lakini pia unaweza kuchanganya na mahindi kwa ajili ya Ugali.