By Naomi Achieng
Mkurungenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), Bwn. David Kafulila amekutana na baadhi ya wanachama wa Chama cha Wamiliki wa Malori wakati na wadogo (TAMSTOA) Ijumaa Novemba 22, 2024 na kuwaeleza fursa mbalimbali za uwekezaji ikiwemo kuwekeza kwenye mabasi ya mwendokasi (BRT)
Bwn. David Kafulila amewashauri wanachama hao kuandaa andiko lao jinsi gani wanaweza kuwekeza, pia uwezo wao ni kununua mabasi mangapi, na huduma nyingine ambazo zipo na wameziona kuwa ni fursa.
“Mradi wa mabasi BRT una awamu sita na tayari wawekezaji wakuwekeza kwenye BRT awamu ya kwanza na ya pili wamepatikana, hivyo TAMSTOA mna fursa ya kuanza kuomba kuwekeza awamu zilizobaki,”alisema David Kafulila.
Mwenyekiti wa TAMSTOA , Chuki Shaban ameishukuru PPPC kwa kuandaa mkutano huo na kuwapa elimu kuhusu elimu ya ubia kupitia PPPC.
“Tunashukuru kukutana hapa leo, na tuko tayari kuwekeza kwenye mradi wa mwendo kasi. Changamoto tunayoina ni ule mchakato mzima wa kuwekeza kwenye,” alisema Chuki Shaban.
Mjumbe wa Kamati kuu ya TAMSTOA Josephat Pallangyo amesema ni vyema utaratibu wa kuwekeza kwa hisa ukatumika kama ilivyo kwa benki ya CRDB au NMB.
Mwisho