UKAGUZI, USAFI WA MADARAJA NA MAKALAVATI.
LINDI

By Naomi Achieng

http://ukaguziiusafi//madaraja//kalavati/tanzania/lindi//

Lindi

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seff  amewaagiza Mameneja  wa TARURA wa Wilaya kote nchini kukagua na kusafisha madaraja na makalavati yote  katika maeneo yao ili yaweze kupitisha maji kwa urahisi na kuepusha mafuriko.

Mhandisi Seff,  ametoa maagizo hayo wakati wa ziara yake mkoani Lindi katika wilaya za Nachingwea, Liwale na Ruangwa na kusema kwamba msimu wa mvua umeshaanza katika maeneo mengi hapa nchi hivyo kwa kufanya usafi huo itasaidia kulinda miundombinu hiyo iliyotumia fedha nyingi za walipa kodi.

“Kila Meneja anapaswa kukagua na kufanya usafi kwenye madaraja na makalavati katika maeneo yake ili mvua zinaponyesha isikwamishe shughuli za kiuchumi na kijamii kwa wananchi endapo madaraja au makalavati yatasombwa  na maji”.Alisisitiza

Naye, Meneja wa TARURA Mkoa wa Lindi Mhandisi Fanuel Kalugendo aliahidi kusimamia na kufuatilia agizo la Mtendaji Mkuu na kutoa taarifa baada ya kazi kukamilika.

Mhandisi Seff yupo ziara ya kikazi ya kufuatilia miradi ya ujenzi na matengenezo ya miundombinu ya barabara mkoani Lindi.