VIFO 13 JENGO LILILOPOROMOKA KARIAKOO,
Dar es Salaam

By Naomi Achieng'

Rais Samia Suluhu Hassani amesema hadi sasa 4:00  asubuhi ya leo jumapili, Novemba 17, 2024 watu 13 wamepoteza maisha na majeruhi 84 kuokolewa katika ghorofa lililoporomoka, Kariakoo jijini Dar es salaam.

Pia ametoa maagizo kwa Waziri Mkuu na Polisi, "Namtaka Waziri Mkuu kuongoza timu ya ukaguzi majengo kuendelea na zoezi la kukagua majengo yote ya Kariakoo tupate taarifa kamili ya hali ya majengo ya karikoo ilivyo. Jeshi la polisi ipate taarifa kamili kwa mmiliki wa majengo ya jinsi ujenzi ulivyokuwa" amesema

Raisi Samia amesema hayo leo Jumapili, akiwa Rio de Janeiro Brazili kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa na kurugenzi ya Mawasiliano ya Raisi Ikulu ya Tanzania. Amesema kati ya majeruhi hao 26 wanaendelea na matibu.

"Serikali itabeba gharama za matibabu kwa waliojeruhiwa na kuhakikisha waliopotexa maisha watasitiriwa ipasavyo, nitoe pole kwa ndugu, jamaa na marafiki", amesema Raisi Samia.

Amesema serikali itaendelea kutoa taarifa zaidi "hadi sasa sababu za kitaalamu za jengo kuporomoka hazijachunguzwa na kubainishwa na kipaumbele chetu ni kufanya uokozi".

Rais Samia amesema taarifa zote hizo zikipatikana zitawekwa wazi na Watanzania watazisikia.

Mwisho.